Michezo

Saruni avunja rekodi mita 800 Desert Heat Classic

April 30th, 2018 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

MICHAEL Saruni aliandikisha rekodi mpya ya mbio za mita 800 ya Riadha za Kitaifa za Taasisi za Elimu ya Juu nchini Marekani na Canada (NCAA) baada ya kutwaa taji la Desert Heat Classic mjini Tucson, Arizona, Marekani, Aprili 28, 2018.

Mwanafunzi huyu wa mwaka wa pili wa Chuo Kikuu cha Texas kutoka Kenya alikamilisha mizunguko hiyo miwili kwa dakika 1:43.25 na kuvunja rekodi ya Muamerika Donovan Brazier, ambaye alitimka umbali huo kwa rekodi ya NCAA ya 1:43.55 mwaka 2016.

Muda wa Saruni wa 1:43.25 pia ni kasi ya juu duniani mwaka 2018. Kabla ya kuandishwa kwa muda huu, Mkenya Jonathan Kitilit ndiye alikuwa amekamilisha mbio za mita 800 mwaka 2018 kwa kasi bora ya dakika 1:44:64 hapo Februari 17, 2018 jijini Nairobi.

Mkenya David Rudisha ndiye mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za mita 800. Alitimka umbali huo kwa dakika 1:40.91 katika Michezo ya Olimpiki jijini London nchini Uingereza mwaka 2012.

Matokeo ya Desert Heat Classic (mita 800):

Michael Saruni (Chuo Kikuu cha Texas) dakika 1:43.25

Carlos Villarreal (Arizona) 1:46.70

Jonah Koech (Chuo Kikuu cha Texas) 1:47.12

Collins Kibet (Arizona) 1:47.83

Hari Sathyamurthy (Stanford) 1:49.93

Brian Smith (Stanford) 1:50.68

Christian White (Stanford) 1:50.97

Ryan Lanley (Northern Arizona) 1:51.07