Habari Mseto

Serena Hotels yafungua tawi jipya DRC

February 7th, 2019 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Hoteli ya Serena imefungua tawi jipya Demokrasia ya Congo (DRC). Kulingana na meneja mkurugenzi wa Serena Bw Mahmud Janmohamed, hoteli hiyo inafungua tawi mjini Goma, mji ambao unafahamika zaidi kwa shughuli za uchimbaji migodi.

Hii ni baada ya kuingia katika kandarasi na hoteli moja mjini humo ambapo hoteli hiyo itaanza kusimamia hoteli hiyo Julai 2019.

Hoteli ya Serena ina operesheni nchini Kenya,Tanzania, Uganda, Rwanda, Unguja na Mozambique.

Bw Janmohamed, anatarajia kuwa idadi ya watalii nchini itaongezeka hasa watalii kutoka ng’ambo.

Mwaka jana, takriban watalii milioni mbili wa kimataifa waliwasili nchini licha ya mwaka kuanza kwa hali ngumu hasa kutokana na uchaguzi mkuu wa 2017.

Lakini tishio la ugaidi huenda likaathiri sekta hiyo hasa kutokana na baadhi ya mataifa kutoa onyo la kiusafiri kwa raia wake.