Serge Gnabry awabeba Bayern Munich dhidi ya Cologne kwenye Bundesliga

Serge Gnabry awabeba Bayern Munich dhidi ya Cologne kwenye Bundesliga

Na MASHIRIKA

SERGE Gnabry alifunga mabao mawili na kusaidia waajiri wake Bayern Munich kupepeta Cologne 3-2 katika mechi ya Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) mnamo Jumapili.

Robert Lewandowski alifungulia Bayern ukurasa wa mabao katika dakika ya 50 baada ya kukamilisha kwa ustadi krosi ya chipukizi Jamal Musiala.

Gnabry alipachika wavuni bao la pili dakika nane baadaye, kabla ya wageni Cologne kusawazisha haraka kupitia mabao mawili ya Anthony Modeste na Mark Uth.

Bayern walipata bao la ushindi kupitia kwa Gnabry katika dakika ya 71.

Lewandowski ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Poland, sasa amefunga katika kila mojawapo ya mechi 12 zilizopita za Bundesliga na kujizolea jumla ya mabao 19 kutokana na michuano hiyo. Mara ya mwisho kwa Lewandowski kuchezea Bayern bila kufunga bao ni Februari 2021.

Ushindi wa Bayern ulikuwa pia wa kwanza kwa kocha mpya Julian Nagelsmann aliyeshuhudia kikosi chake kikiambulia sare ya 1-1 dhidi ya Borussia Monchengladbach katika mchuano wa kwanza wa Bundesliga msimu huu.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

TAHARIRI: Heko chipukizi kuitawala dunia

Serikali kutafutia bandari biashara