Siasa

Serikali inataka kubomoa Weston Hotel kumzima Ruto 2022 – Ahmednasir Abdullahi

October 5th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

NAIBU RAIS Dkt William Ruto amesema siasa za kinyang’anyiro cha urais hapo 2022 ndizo kiini cha mahakaMa kutaka hoteli yake ya Weston ibomolewe. 

Mawakili wa hoteli hiyo wamewasilisha stakabadhi mpya mahakamani wakisema kesi hiyo imeingizwa siasa na Mamlaka ya Usafiri wa Ndege nchini (KCAA) inayoshirikiana na wanasiasa fulani kuchafua jina la Dkt Ruto.

The hotel has filed fresh court papers arguing that the suit is a conspiracy between the Kenya Civil Aviation Authority (KCAA) and certain political actors to politicise the controversial land deal for cheap political drama.

“Ni jaribio la wanasiasa kumharibia Naibu Rais jina kwani wanajua amewekeza katika sehemu ya hoteli hiyo ,” anasema wasilisho la wakili wa hoteli hiyo Ahmednasir Abdullahi.

KCAA inataka leseni ya hoteli hiyo ifutwe, halai ambayo itapelekea kubomolewa kwake.  Imepinga uamuzi wa mahakama kuwa Tume ya Ardhi nchini (NLC) kuwa Weston inafaa kuendelea kumiliki ardhi hiyo na kuififia KCAA kwa bei ya sasa ya soko.

“Ni njama tu ya kumchafulia sifa Dkt Ruto kisiasa. Ni kwa sababu ya njama hiyo ya kisiasa ambapo KCCA ililazimishwa kuwasilisha pingamizi hizi badala ya kukata rufaa kutona na uamuzi wa korti kuhusu NLC,” akasema Bw Abdullahi.