Serikali kutoa mwelekeo wa kalenda ya masomo

Serikali kutoa mwelekeo wa kalenda ya masomo

NA SAMMY KIMATU

SERIKALI itatoa mwelekeo wa jinsi masomo yatakavyoendelea punde korti ya upeo itakapoamua kesi ya kupinga matokeo ya kura ya urais ikiwa kutakuwa na mabadiliko.

Waziri wa Elimu, Prof George Magoha alisema hayo Jumatano wakati alikuwa akiwahutubia wanahabari jijini Nairobi na kusisitiza kwamba shule zote zinafunguliwa leo Alhamisi.

Aliongeza kwamba ikiwa kutakuwa na upigaji kura siku nyingine, wanafunzi hawatakubaliwa kuondoka shuleni.

Badala yake, alisema watoto wataruhusiwa kubakia katika bweni au wapewe nafasi kucheza.

Prof Magoha aliongeza kwamba shule zinatarajiwa kufungwa kwa likizo ya muhula wa pili Agosti 30.

Aidha, alisema ikiwa kutakuwa na mabadiliko katika kalenda ya elimu, wizara yake itawashirikisha washikadau wote ili waafikiane kwa kauli moja.

Isitoshe, Prof Magoha aliwaomba wananchi wapatie wizara nafasi ifanye kazi yake wakati huu taifa linaposubiri kujua hatma ya uamuzi wa korti baada ya Bw Raila Odinga kuahidi kwenda mahakamani.

“Siasa, uchaguzi na janga la corona ni baadhi ya changamoto zilizoathiri kwa kuvuruga kalenda ya masomo,” Prof Magoha akasema.

Kwa manufaa na faida ya mtoto, alisema kuna umuhimu wa usalama wa mtoto kupewa kipaumbele na kuongeza kwamba wizara ya elimu itashirikiana na zingine kikazi.

Akiwachekesha wanahabari, Prof Magoha alisema anaomba msamaha kwa mtu yeyote aliyekerwa na matamshi au semi zake akiwa kazini, akiongeza kwamba yeye hupenda mzaha na asieleweke vibaya.

Aliongeza kwamba juhudi za kuongoza wizara ya elimu zimezaa matunda kutokana na uwezo wa Mwenyezi Mungu wakati wa utawala wa rais Uhuru Kenyatta na naibu wa rais Dkt Samuel Ruto.

Vilevile, alifichua kwamba yuko safarini kwenda nyumbani pamoja na rais Uhuru Kenyatta akimaliza muhula wake uongozini.

Alisema kujituma kwake kazini kunatokana na wito wa shule yake ya zamani ya Starehe Boys Centre ya “Tulenge Juu, Hatuogopi.”

  • Tags

You can share this post!

Chebukati afichua njama kali ya Cherera na wenzake

VALENTINE OBARA: ODM ijipige msasa ndipo iweze kuendelea...

T L