NA WINNIE ATIENO
SERIKALI inanuia kuhalalisha waganga wa tiba ya kiasili na wakunga katika juhudi za kuimarisha sekta ya afya nchini.
Waziri Msaidizi wa Afya, Rashid Aman amesema mpango huo pia utakuza matumizi ya tiba asilia na kuwapa wataalamu wake mapato.
Alisema wanabuni sheria ambayo itasimamia tiba hiyo ya kiasili.
Hata hivyo alionya Wakenya kutofautisha waganga wa tiba asili na wachawi.