Serikali yafungua kituo kudhibiti uvamizi wa nzige

Serikali yafungua kituo kudhibiti uvamizi wa nzige

NA COLLINS OMULO

SERIKALI imeimarisha juhudi za kuzuia uvamizi wa nzige siku zijazo kwa kufungua kituo maalum cha utafiti ambacho kitakuwa kikitoa onyo kuhusu ujio wa wadudu hao.

Waziri wa Kilimo, Mithika Linturi jana Alhamisi alisema kuwa kituo hicho cha utafiti kitasaidia kutambua dalili za mapema zinazoashiria uvamizi wa nzige unanukia kisha kuchukua hatua za kunusuru hali ili kuwaepushia wakulima hasara.

Mnamo 2020, uvamizi wa nzige ulichangia kuharibiwa kwa ekari kadha ya mashamba yaliyokuwa na mimea kwenye kaunti 24 nchini. Bw Linturi alisema kituo hicho kimejengwa kupitia ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Chakula na Kilimo (UNFAO).

Waziri huyo alimwomba Mkurugenzi Mkuu wa UNFAO Dkt Qu Duoyng ahakikishe kuwa wanasaidia Kenya kuandaa Kongamano la Kimataifa la Kupambana na Nzige Mnamo Machi 2023.

  • Tags

You can share this post!

Mbunge ataka wakongwe walindwe kwa njia bora

Wanaharakati kortini kupinga Hazina ya Hasla, wataka...

T L