Serikali yaonya wasafiri kuhusu magaidi

Serikali yaonya wasafiri kuhusu magaidi

NA MANASE OTSIALO

SERIKALI imetahadharisha wakazi wa Mandera wasio wa asili ya Kisomali dhidi ya kutumia barabara ya Mandera-Rhamu-Elwak-Kotulo-Wajir.

Hii ni baada ya abiria wasio wa asili ya Kisomali kulengwa na wanaoshukuwa kuwa wanachama wa kundi la Al-Shabaab.

Sasa itawalazimu watu wasio wenyeji kusafiri kwa ndege au kutumia barabara ndefu ya Mandera-Rhamu-Banisa-Moyale kuingia au kutoka Mandera.

Mnamo Jumatano, wasafiri waliokuwa wakielekea mjini Mandera walishikwa mateka na magaidi hao na kuzomewa kwa muda wa saa mbili.

Kwa mujibu wa ripoti iliyoandikishwa katika Kituo cha Polisi cha Kotulo, idadi isiyojulikana ya magaidi wa kundi la al-Shabaab waliojihami vikali walisimamisha basi la abiria linalomilikiwa na kampuni ya Al-Mukaram katika eneo la Lag Mata Kuta kati ya mji wa Dabacity na Dimu hill viungani mwa Mandera Kusini.

Dereva wa teksi na bodaboda walizuiliwa pia.

  • Tags

You can share this post!

Kampuni yakanusha madai ya ubaguzi wa rangi kwa waajiriwa

Obiri atawala 10,000m Kasarani, zamu ya Omanyala ni leo...

T L