Serikali yazima matumaini ya michezo kurejelewa

Serikali yazima matumaini ya michezo kurejelewa

Na MWANGI MUIRURI

SERIKALI imepuuzilia mbali habari za awali kuwa kuna uwezekano wa michezo kuerjelewa humu nchini, iksema masharti ya kudhibiti corona yataendelea akama yalivyotangazwa.

Jumatano asubuhi, Naibu Waziri wa Spoti Bw Zack Kinuthia Jumatano alikuwa ametoa matumaini kuwa huenda harakati za kispoti ziondolewe marufuku ya rais Uhuru Kenyatta aliyoyatoa Ijumaa iliyopita kama njia ya kupambana na janga la Covid-19.

Bw Kinuthia alikuwa amesema kuwa “kwa kila utathimini kama wizara tuna uhakika kwamba sekya ya kispoti imejimudu kuzingatia usalama wa hali ya juu dhidi ya janga hili na tumependekezea rais ayaondoe marufuku hayo.”

Hata hivyo, Naibu huyo wa waziri akihutubu katika kaunti ya Murang’a alisema kuwa uamuzi wa mwisho unaweza tu akatekelezwa na rais “letu likiwa tu ni kufikisha ujumbe wetu unaotokana na mikutano ya mashauriano na wadau katika sekta hii, jukumu ambalo tu,melitekeleza na tungoja habari njema kutoka Ikulu.”

Kando na marufuku hayo ya Kispoti, Rais alizima mikutano ya kisiasa, kongamano katika jamii, harusi ikazimiwa mashahidi wa kuhudhuria hadi 15, mazishi ya wafu yakielekezwa yawe yakiandaliwa chini ya masaa 72 baada ya kuaga dunia na waombolezaji wasizidi 50, magari ya uchukuzi wa umma yawe yakibeba asilimia 60 ya uwezo wayo na hatimaye Kaunti za Nairobi, Nakuru, Machakos, Kajiado na Kiambu zikafungiwa kutangamana na zingine 42.

Bw Kinuthia aidha alisema kwamba wizara yake inasukuma kuzinduliwe sera maalum ya kuongoza upimaji na matibabu ya wanaspoti dhidi ya Covid-19.

Alisema kuwa kwa sasa mikakati iliyoko haina ulainifu na haina ule uadilifu unaohitajika.

Bw Kinuthia alisema kwamba kunafaa kuwe na utaratibu wa vipimo na matibabu akiguzia kwamba leo hii, wanaspoti wanashirikishwa harakati hizo kwa njia ya kuharakishwa, yenye haina usiri na uhakika wa kuchukua waathiriwa kama mashujaa wa taifa hili ambao wanafaa kupigwa jeki na serikali.

Alisema kuwa harakati za kuwachanja wanaspoti zitazinduliwa hivi karibuni kabla ya warejeshewe uhuru wa kujumuika nyugani akisema anatarajia maazimio hayo yatimie hivi karibuni.

You can share this post!

Cape Verde, Guinea-Bissau, Mauritania na Ethiopia pia...

TANZIA: Mbunge wa Kiambaa Paul Koinange afariki kutokana na...