Serikali yazindua rasmi mbolea ya bei nafuu

Serikali yazindua rasmi mbolea ya bei nafuu

NA SAMMY WAWERU

NAIBU Rais Rigathi Gachagua amezindua rasmi mpango wa mbolea ya bei nafuu kuanza kusambazwa kote nchini.

Hatua hiyo inatokana na tangazo la Rais William Ruto baada ya kuapishwa Septemba 13, 2022 ambapo aliahidi kuwa serikali yake itazindua fatalaiza ya bei nafuu.

Alisema mpango huo ukitekelezwa utasaidia kushusha gharama ya chakula, kupitia utoaji wa ruzuku kupunguza bei ya mbolea.

Akiutetea, Dkt Ruto alisema wakulima wakipunguziwa gharama ya uzalishaji mazao yatakuwa mengi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi jijini Nairobi, Bw Gachagua amewataka wakulima kuendea mbolea hiyo katika mabohari ya Bodi ya Nafaka na Mazao Nchini (NCPB).

“Serikali imefanya majadaliano na wadauhusika kuhakikisha bei inayosambazwa imeafikia ubora wa bidhaa na ni ya bei tuliyoweka,” Naibu Rais akasema.

Hata kabla ya uzinduzi rasmi, baadhi ya maeneo nchini yalikuwa yameanza kupokea.

Magunia milioni 1.4 ya kilo 50 yatasambazwa kote nchini.

Gachagua alisema serikali imetoa kima cha Sh3.55 bilioni kufanikisha mpango wa ruzuku ya mbolea.

Mfuko wa fatalaiza ya DAP utamfikia mkulima kwa Sh3, 500 bei ya chini kutoka Sh7, 000, CAN Sh2,875, NPK Sh3,275, huku MOP ikiwa Sh1,775, na UREA na Sulphate of Ammonia ikiuzwa Sh3,500 na Sh2,220 mtawalia.

“Mbolea hii itawafaa wakulima wanaopanda msimu huu wa mvua fupi,” Gachagua akasema.

Fatalaiza hiyo hata hivyo inasambazwa wakati ambapo wakulima wengi nchini wameshafanya shughuli ya upanzi.

Wanahimiza serikali kuwasambazia mbolea ya kunawirisha mazao.

Gharama ya juu ya pembejeo imekuwa kero katika sekta ya kilimo.

  • Tags

You can share this post!

Bandari: Azimio, KK wakwaruzana

Nassir ateua aliyekuwa katibu wa KMPDU kuongoza kamati ya...

T L