Serikali za Uganda, Kenya zakubaliana kusitisha sheria tata za ununuzi

Serikali za Uganda, Kenya zakubaliana kusitisha sheria tata za ununuzi

Na AGGREY MUTAMBO

SERIKALI za Uganda na Kenya zimekubaliana kusitisha utekelezaji wa sheria ya kuagiza mazao ya kilimo kufuatia mkutano baina ya mawaziri wa nchi hizo mbili jijini Nairobi.

Serikali hizo zimesema hazitaweka vikwazo kwa ununuzi wa vyakula va kuku, huku wakitayarisha mpango wa sera wa muda mrefu wa kuondoa vikwazo hizo. Hata hivyo, serikali ya Kenya ilipendekeza ukaguzi mpya wa mchakato wa usindikaji wa maziwa ufanywe upya ili kutathmini ubora wake na kuthibitisha ikiwa uzalishaji ulikuwa wa ndani.

Waziri wa Kilimo nchini, Peter Munya na mwenzake wa Biashara, Betty Maina walikutana na Waziri wa Kilimo wa Uganda, Frank Tumwebaze na kukubaliana kuondoa vikwazo hivyo ambavyo vimeathiri biashara kati ya nchi hizo mbili.

Kadhalika, nchi hizo mbili zilikubaliana kuviondoa vikwazo vinavyoathiri biashara za EAC ifikapo Juni mwaka ujao.

You can share this post!

TAHARIRI: Serikali iweke sera za kudhibiti kupandisha nauli

Wasio na vyeti vya chanjo kukosa huduma za serikali

T L