Sh20m kutumiwa kukarabati jengo la makavazi

Sh20m kutumiwa kukarabati jengo la makavazi

NA KALUME KAZUNGU

MAKAVAZI ya Kitaifa nchini (NMK) kwa ushirikiano na Ubalozi wa nchi ya Oman, imeanzisha ukarabati na uboreshaji wa jengo la Makavazi ya Lamu kwa kima cha Sh20 milioni.

Jengo hilo liko kwenye mji wa kale wa Lamu.Katika mahojiano na Taifa Jumapili ofisini mwake Alhamisi, Afisa Msimamizi wa turathi za kitaifa na Makavazi ya Lamu, Mohamed Ali Mwenje alisema mradi huo utachukua miezi mitano na umepangwa kukamilika kufikia Machi, 2022.

Bw Mwenje alisema ukarabati wote unaoendelea wa jumba hilo la Makavazi ya Lamu unafadhiliwa na Ubalozi wa Oman ulioko jijini Nairobi.Makavazi ya Lamu yalianzishwa mwaka 1970, ambapo yamehudumu eneo hilo kwa karibu miaka 51.Bw Mwenje alisema ukarabati huo utaleta taswira mpya na kuvutia wageni zaidi kutembelea eneo hilo kujifahamisha kuhusu historia ya Lamu,

Pwani na mwambao wa Afrika Mashariki kwa ujumla.“Katika kipindi chote cha miaka 51 ambapo jumba hili limehudumu, hakuna ukarabati wowote uliotekelezwa. Nafurahi kwamba Ubalozi wa Oman hapa nchini umeafikia kutekeleza ukarabati na uboreshaji wa jumba letu la makavazi na tayari kazi imeanza.

Punde ukarabati utakapokamilika utaleta sura mpya na kuvutia

You can share this post!

Serikali haitaweka vikwazo dhidi ya wageni kuingia Kenya...

Mimba za mapema zapungua

T L