Shabana waomba uungwaji mkono

Shabana waomba uungwaji mkono

Shabana waomba usaidizi kutoka kwa mashabiki, huku wakiwasili Nairobi kwa mechi.

NA JOHN ASHIHUNDU

Katibu Mtendaji wa Shabana FC, Stephen Kiama amewaomba mashabiki na wadau wa klabu hiyo ya Supa Ligi ya Taifa (NSL) waendelea kuiunga mkono ili iweze kufanya vizuri msimu huu.

Kiama amedai kwamba kikosi hicho kinachonolewa na Robert Ojienda kina vijana wenye uwezo wa kuirejesha timu hiyo katika Ligi Kuu ya Kenya (FKF-PL) msimu ujao baada ya kukaa nje kwa miaka 23 tangu ishuke mnamo 2006.

Kiama alisema hayo baada ya kikosi kutoka Kisii kuwasili Nairobi kwa mechi yao dhidi ya Kenya Police itakayochezewa Camp Toyoyo kuanzia saa tisa.

Wakati huo huo, kocha wa Muranga SEAL, Vincent Nyaberi ametoa onyo kali kwa wapinzani wao Coast Stima watarajie mtihani mkubwa timu hizo zitakapokutana katika uwanja wa St Sebastian Park, Murang’a.Kocha huyo alisema kufanya vibaya kwa kikosi hicho kabla ya ujio wake hakukumaanisha kwamba ni kibovu kama baadhi ya wadau wanavyosema.

Nyaberi alijiunga na timu hii ikiwa na pointi moja tu baada ya kujibwaga uwanjani mara nane, lakini katika mechi walizocheza chini yake, wamefikisha pointi 23, na iwapo wataibuka na ushindi kesho dhidi ya Kenya Police, watatinga 10 bora jedwalini.

Baada ya sare ya kutofungana majuzi dhidi ya Modern Coast Rangers, kocha huyo alisema: “Kutoka sare, kushinda au kushindwa ni matokeo kimchezo, bali kikubwa ni mashabiki wasivunjike moyo. Timu ipo vizuri baada ya kuifanyia marekebisho.”

Ratiba ya mechi za leo Jumamosi ni:

Gusii FC na Mwatate United (Green Stadium, Awendo), Kenya Police na Shabana (Camp Toyoyo), Murang’a SEAL na Coast Stima (St Sebastian Park), Kisumu All Stars na Modern Coast Rangers (Moi Stadium, Kisumu), Silibwet na Nairobi Stima (Bomet Stadium), APS Bomet na Soy United (Bomet Stadium).

  • Tags

You can share this post!

Moto wateketeza nyumba zaidi ya 100

Spika ataka Yatani akamatwe kwa kukaidi seneti