Mashairi

SHAIRI: Corona janga hatari, limetunyima raha

April 8th, 2020 1 min read

 

Kila mbwa ana siku, kauli ya wahenga,

Kwamba corona janga, ni pigo la Rabana,

Moshi wa huzuni, umeilemaza dunia,

Hatuna hata furaha, tumekunyata tumejikunja.

 

Kusini kaskazini, wote wanalia corona,

Idadi zaongezeka, wagonjwa wanaotuacha,

Pasi hata kuwaaga, wasiwasi unaongezeka,

Kweli kipya kinyemi, janga hili ni kidonda.

 

Yote tisa haya kumi, kunayo matumaini,

Japo ukikatwa muwa, mwingine utachipuka,

Corona imeleta mapya, ujumbe mitandaoni,

Hatuhitaji kwenda kazini, maisha kabadilika.

 

Walakini juu ya yote, mapenzi yameoteshwa,

Huba na mahaba, wapenzi wanamumunya,

Karantini kwa nyumba, makapera wameoa,

Mabinti wasio penzini, huu msimu wa ndoa.

 

Hakika baniani mbaya, kiatu chake dawa,

Safari ni hatua, mapenzi yahitaji dua,

Wanandoa walishane, penzi bila taabu,

Nao wapenzi wachanga, wasubiri janga lipite.

 

©?GamooPoet