Bambika

Shakib: Kama si pesa, penzi langu na Zari lingeyumba

Na SINDA MATIKO June 21st, 2024 1 min read

SHAKIB Lutaaya, ambaye ni mume wake soshiolaiti Zari Hassan, amedai kuwa kama sio uwezo wa kifedha, ndoa yao ingeyumbayumba.

Shakib anaishi Uganda naye Zari akiwa anaishi Afrika Kusini huku kila mmoja akiwa hayupo tayari kuhamia nchi ya mwenzake.

Hii ni kwa sababu Shakib anazo biashara zake anazoendesha Uganda huku Zari naye akiwa na biashara zake anazosimamia Afrika Kusini.

Kutokana na umbali huo, imewalazimu wawili kuja na mbinu ya kuhakikisha penzi lao halivuji na kulingana na Shakib, kwa bahati nzuri uwezo wao wa kifedha umewasaidia sana.

“Naishi Uganda, na yeye anaishi Afrika Kusini ila ninaweza kumwona wakati wowote naye pia vile vile maana tuna uwezo wa kugharamia nauli za usafiri wa ndege muda wowote. Sidhani ni jambo baya kwa watu ambao wanafanya kazi,” anasema Shakib.

Aidha Shakib anasema anapenda mpangilio huo kwani kama ingelikuwa ni kuishi pamoja basi wangeishia kuchokana haraka kutokana na kuzoeana.Ila umbali wao unawafanya wote kuwa na hamu ya kuonana.