Sharti uchaguzi uwe wa amani -Matiang’i

Sharti uchaguzi uwe wa amani -Matiang’i

Na RUTH MBULA

MAWAZIRI watatu jana walisema watamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta kikamilifu kwa kuhakikisha wanafanya lolote wawezalo kuhakikisha uchaguzi mkuu ujao umeendeshwa kwa njia ya amani.

Mawaziri Fred Matiang’i (Usalama wa Ndani), Joe Mucheru (ICT) na Mutahi Kagwe (Afya), walisema kumbukumbu za ghasia za uchaguzi tata wa 2007 bado zingalipo.Hivyo, walisema hawatakubali Kenya kujipata katika hali hiyo tena.

Dkt Matiang’i alisema nchi inapaswa kuwa thabiti, akieleza si vigumu Kenya kujipata katika hali sawa na Somalia ama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiwa hatua zifaazo hazitachukuliwa kuhakikisha uwepo wa amani.

“Tunaweza kuwa na changamoto kama umaskini, maradhi kati ya nyingine nyingi. Hata hivyo, amani na umoja wa nchi ni nguzo muhimu,” akasema.Alisema uchumi wa nchi utakua tu ikiwa kutakuwa na amani.

“Lazima tusikize vile Rais anavyotwambia. Ana nia njema kwetu. Tunajua hilo kwani tunaona anakotupeleka,” akasema.Alisema eneo la Gusii linahitaji amani, kwani idadi kubwa ya wenyeji wanaishi katika sehemu mbalimbali nchini.

Mawaziri hao walikuwa wakihutubu jana kwenye hafla ya kuchangisha pesa katika Shule ya Msingi ya Nyaura DEB, iliyo katika eneobunge la Nyaribari Chache, Kaunti ya Kisii.Miongoni mwa waliohudhuria ni mkewe kiongozi wa ODM, Raila Odinga, Bi Idah Odinga, wabunge Richard Tong’i (Nyaribari Chache), Lilian Gogo (Rangwe), Simba Arati (Dagoretti Kaskazini) kati ya wengine.

You can share this post!

Kotut atawala mbio za Italia baada ya ukame wa miaka 3

Mutua aahidi wanandoa ‘zawadi’ ya Sh0.5 milioni...

T L