Bambika

Shepu yangu si ya kubandika, ni maumbile asili, asisitiza Trisha Khalid

May 31st, 2024 1 min read

NA SINDA MATIKO

MWIGIZAJI na mtengenezaji maudhui Trisha Khalid anasema kachoka kujieleza kuhusu shepu yake.

Toka alipochipuka kama TikToker 2020 kabla ya kuishia kuwa mwigizaji mkubwa, shepu ya kutamanisha ya Trisha imekuwa ikizua gumzo sana hasa mitandaoni.

Wengi wamedai kuwa shepu yake mwanana ya kiuno chake cha nyigu na neema ya alivyojazia jazia maeneo ya chini, yatokana na yeye kufanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio.

“Nimeshajieleza kuhusu hili suala na sidhani nitajieleza tena, wanachotaka kusema watu kuhusu shepu yangu basi na waseme tu,” anasema Trisha.

Mrembo huyo ameishi kusisitiza kuwa shepu yake ni maumbile akisema kuwa alirithi maumbile yake mwanana kutoka kwa mamake mzazi.

Aidha, Trisha anasema huwa anajitahidi sana kufanya mazoezi ili kulinda shepu yake jambo ambalo wengi wanashindwa kuamini na kudai kabandika makalio.