Habari Mseto

Shetani asisingiziwe kwa ubakaji – Hakimu

June 16th, 2019 1 min read

Na Kalume Kazungu

HAKIMU katika mahakama ya Lamu amewataka wahalifu wakome kumsingizia shetani wanapovunja sheria.

Hakimu Mkuu, Allan Temba, anasema kumekuwa na ongezeko la tabia ya wahalifu hasa wale wa ubakaji na ulawiti ambao wamekuwa wakikimbilia kumlaumu ibilisi wanaposimamam kizimbani kwa madai kwamba ni huyo shetani au ibilisi ndiye huwasukuma kufanya vityendo vyao viovu.

Akizungumza alipokuwa akitoa hukumu kuhusiana na kesi ya ubakaji iliyokuwa ikihusisha kiongozi wa dini, Ustadh Salim Issa Abdalla, 39, alisema shetani hatambuliwi kwenye sheria za Kenya na kwamba wanaofanya makosa lazima wajutie makosa yao kama watu binafsi.

“Sheria ya Kenya haimtambui shetani au ibilisi na hii ndiyo sababu hakuna kifungo chochote cha shetani. Wahalifu wanapofanya makosa lazima wajutie makosa hayo kwani kujaribu kumsukumia shetani ni jambo lisilofaa,”alisema.

Ustadh Salim Issa Abdalla,39, akiwa kizimbani kwenye mahakama ya Lamu. Alikuwa ameomba mahakama kumuonea huruma kwani shetani au ibilisi alikuwa amemsukuma kufanya ubakaji. Picha/ Kalume Kazungu

kwani shetani hana hatia katika kitendo chako ulichofanya cha ubakaji. Korti inakufunga miaka 20 gerezani kwa kosa hilo na uko na siku 14 za kukata rufaa,” akasema Bw Temba.

Katika kesi nyingine, mwanamume wa miaka 26 alifungwa maisha baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti nduguye wa kambo wa umri wa miaka 11.

Bw Yahya Hussein alikuwa ameshtakiwa kwamba mnamo Mei 17 mwaka jana, katika kijiji cha Mokowe, alimdhulumu kakake wa kambo kwa kumlawiti na kisha kumtisha kutofichua uovu huo.