Shikanda ashukuru Ingwe kumwamini

Shikanda ashukuru Ingwe kumwamini

NA JOHN ASHIHUNDU

MWANASOKA mstaafu, Dan Shikanda amewapongeza wanachama wa AFC Leopards kwa kumchagua tena kusimamia klabu hiyo kwa miaka mitatu.

Shikanda ambaye miaka ya 90s aliwahi kuchezea Leopards na Gor Mahia pamoja na Harambee Stars alichaguliwa mwishoni mwa wiki kwa mara ya pili, baada ya kumbwaga Ronald Namai kwa kura 429 dhidi ya 282.

Katika uchgauzi huo uliofanyika katika uwanja wa kimataifa wa Kaasarani na kusimamiwa na Frank Mukwanja, chini ya uangalizi mkubwa wa Msajili wa Vyama vya Michezo, Rose Wasike, mashabiki hao wa Ingwe walimchagua Gilbert Andugu kama Katibu mpya wa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Kenya.

Andugu ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa matawi ya klabu hiyo aliwashinda Robert Situma na Tonny Omusina baada ya kupata kura 395. Situma alipata 190, huku Omusina akiridhika na 42.

Oliver Napali alichaguliwa kuwa Mweka Hazina bila kupingwa, baada ya mpinzani wake pekeee Maurice Chichi kupigwa marufuku kuwania wadhifa huo kutokana na hitilafu kwenye makaratasi yake.

Shikanda aliwashuru wanachama kwa kuamini uongozi wake, licha ya matatizo mengine yaliyokumba klabu hiyo katika muhula uliopita hasa baada ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

“Asenteni sana kwa kuniunga mkono, hata wakati mambo yalikuwa magumu. Kadhalika ningependa kuwapongeza wachezaji wetu kwa kujitahidi kwenye hali hiyo ngumu na kumaliza katika nafasi ya tano ligini,” alisema Shikanda.

“Uchaguzi umekwisha, sasa jukumu lilipo mbele yetu ni kushirikiana ili klabu ipate ufaninsi zaidi. Ningependa tuanze hii safari pamoja ili nitekeleze ahadi zote ambazo nilizitoa wakati wa kampeni. Wakati wa muhula wangu wa kwanza, tulifanikiwa kupata ardhi yetu nje ya uwanja huu ambayo ilikuwa imevamiwa na maskwota. Ningependa kuwahakikishia mashabiki wa Ingwe kwamba nitajitahidi kuhakikisha timu imerejesha hadi yake ya zamani,” aliongeza.

Mgombeaji wa wa kiti cha Ugavana Nairobi, Polycarp Igathe aliyefika kituoni kushuhudia kura hizo zikipigwa aliahidi kutafutia Leopards wadhamini huku akiwahakikishia mashabiki kwamba atagharamia mafuta ya basi la kusafirisha wachezaji wa Ingwe kuanzia msimu ujao.

  • Tags

You can share this post!

JIJUE DADA: Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi na kwa muda...

DKT FLO: Kiharusi cha joto ni maradhi gani?

T L