Shikangwa achangia bao Karagumruk ikiendelea kutesa wapinzani Ligi Kuu Uturuki

Shikangwa achangia bao Karagumruk ikiendelea kutesa wapinzani Ligi Kuu Uturuki

Na GEOFFREY ANENE

JENTRIX Shikangwa alitetemesha nyavu za Adana mara moja huku timu yake ya Fatih Karagumruk ikiandikisha ushindi mwingine muhimu wa mabao 3-0 uwanjani Muharrem Gulergin, Jumamosi.

Mshambulizi huyo Mkenya amekuwa akichangia mabao na pia kusuka pasi zilizozalisha mabao tangu ajiunge na Karagumruk kutoka Vihiga Queens mwezi Januari. Mchango wake umeshuhudia Karagumruk ikijiweka pazuri kumaliza Kundi B katika mduara wa nne-bora wa kufuzu kushiriki robo-fainali.

Karagumruk inakamata nafasi ya pili katika kundi lake kwa alama 39. ALG Spor imekaa juu ya kundi hilo la klabu 12 kwa alama 47. Hakkarigucu na Konak, ambazo zinashikilia nafasi mbili za mwisho za kuingia robo-fainali, zimezoa alama 37 na 36 mtawalia. Timu zote zimesakata michuano 17. Inasalia mechi tano msimu wa kawaida utamatike.

Kundi A linaongozwa na Besiktas kwa alama 45 ikifuatiwa na Fenerbahce (43), Fomget (35) na 1207 Antalya (35). Timu nne za kwanza kundi makundi hayo mawili zitaingia awamu ya muondoano. Mabingwa watetezi ni Besiktas.

You can share this post!

Freiburg wataka Bayern waadhibiwe kwa kuchezesha wanasoka...

NTSA yafunga mtandao wa leseni kwa shule za udereva

T L