Habari Mseto

Shilingi ya Kenya yaimarika zaidi

August 17th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

LICHA ya changamoto zinazoshuhudiwa nchini, shilingi ya Kenya imesalia dhabiti zaidi ikilinganishwa na sarafu nyingine ulimwenguni.

Kwa sasa, shilingi ya Kenya ni ya tatu kati ya sarafu zinazofanya vyema zaidi ulimwenguni, hasa kutokana na mauzo ya nje ya bidhaa za kilimo na utalii.

Kwa sasa, kiwango cha watalii waliozuru nchini hasa kutazama kuvuka kwa nyumbu kutoka Serengeti (Tanzania), kuingia katika Mbuga ya Wanyamapori ya Serena kimekua sana kikilinganishwa na miaka mingine kulingana na Wizara ya Utalii.

Pia, watalii wamefurika katika mji wa Watamu kutazama nyangumi wakivuka. Mandhari ya kisiasa nchini Kenya pia yameimarika sana, hasa baada ya maafikiano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Kwa sasa, dola ya Marekani ni Sh100.86 za Kenya.