Habari Mseto

Shindano la Leba Dei: Tuma picha ukiwa na mwenzako kazini mjishindie Sh5,000

May 1st, 2018 1 min read

Na CHRIS ADUNGO

JUMANNE hii Sh5,000 zitatolewa kwa washindi watatu bora, mmoja kutoka Facebook, mwingine kupitia Twitter na watatu kwa Instagram.

Mshindani anatakiwa kueleza kuhusu rafiki yake wa kazini katika Kiswahili mufti. Wawili hao pia watashinda pesa hizo kisha wagawane.

 

Jinsi ya kushiriki

Je, una rafiki eneo lako la kazi ambaye unapenda kufanya kazi naye?

Je, anakusisimua na kukufanya ufurahie kazi yako zaidi?

Leba Dei hii, Taifa Leo inakupa nafasi ya kusherehekea furaha anayokupa rafiki yako wa kazini na kukuzawadia kwa kumthamini kwa  kufanya kazi yako iwe rahisi. Kushiriki, fuata maagizo haya:

1.     Piga picha au utafute picha ya pamoja ukiwa mfanyikazi mwenzako unayemthamini

2.     Tuelezee ni kwa nini unamthamini rafiki yako huyo kwa kutumia lugha mufti

3.     Pachika picha hiyo mitandaoni kwenye majukwaa yetu (Facebook, Twitter na Instagram)  ukianza na hashtegi #bidiiizawadiwe na kumalizia kwa #KiswahiliKisikike

Washindi watatangazwa mitandaoni. Kila la heri.