Habari Mseto

Shinikizo viongozi wafisaadi SDA wakamatwe

September 4th, 2019 2 min read

BENSON AYIENDA na JOSIAH ODANGA

WAWAKILISHI wa kundi lilojitenga kutoka Kanisa la Kiadventista (SDA), Nairobi Cosmopolitan Conference (NCC) lililoko Kisii limezitaka taasisi husika za serikali ziwakamate maafisa wanaodaiwa kuwa wafisadi.

Wamezitaka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kuchukua hatua za haraka kurejesha sura ya kanisa hilo ambalo limeharibiwa na uovu huo.

Wakiongozwa na maafisa wao, Mbw George Morara Simi na Kennedy Mogire, walilalamika kuwa kanisa hilo limegeuzwa kuwa ngome ya ufisadi.

“Hatupiganii nyadhifa za juu za uongozi kanisani lakini tunahimiza uwepo wa uwazi na uwajibikaji. Kile tunataka na mabadiliko katika uongozi wa kanisa,” Bw Morara akaambia “Taifa Leo”.

Viongozi hao ambao wanalenga kuwaondoa wanachama kutoka kundi la Central Kenya Conference (CKC) ambalo wanachama wake wanadaiwa kuiba pesa za umma, wanasema nia yao ni kuona masuala ya kanisa hilo yakiendeshwa kwa uwazi.

Wakati huu, kundi la NCC lina wakurugenzi watatu na kundi la wahudumu wa kujitolea. Maafisa hao wanashikilia afisi hizo kwa muda hadi uchaguzi rasmi utakapoendeshwa na mwanachama wa kundi katika tarehe itakayotangazwa baadaye.

Tayari wamefungua akaunti za benki, ambako wanachama wameshauriwa kuelekeza malipo yao ya fungu la kumi badala ya kuelekeza fedha hizo kwa kundi la CKC.

Mbw Morara na Mogire waliambia Taifa Leo kwamba hatua waliochukua inafaa wakiongeza kuwa wameigatua kutoka Nairobi hadi eneo la Gusii.

“Nawahimiza Waadvetisti na Wakristo wenye nia njema kusimama kidete na kupinga ufisadi serikalini na ndani ya Kanisa. Ikiwa tutaruhusi ufisadi kanisani basi maadili yataporomoka,” pasta Mogire, ambaye ni mwanachama wa Kanisa la Gekomu SDA ya Jumuiya ya Kenya Kusini, akasema.

Hatua hii ya kundi lenye “itikadi tofauti” ina maana kuwa ghasia zilizoshuhudiwa katika Kanisa la Nairobi Central (Maxwell) na Kanisa la Mautain View zitasambaa hadi eneo la Gusii ambako SDA imekita mizizi.

Mapasta hao wawili walisema hataongoza ibada tofauti kwa sababu kanisa la SDA ni moja