Michezo

Shinikizo zamlazimu mamake Neymar kutema mpenzi mpya shoga

April 26th, 2020 2 min read

GEOFFREY ANENE Na CHRIS ADUNGO

MAMAYE supastaa wa Paris Saint-Germain Neymar, Nadine Goncalves amekatiza uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake mwenye umri wa miaka 23 siku 10 tu baada ya kuuanzisha.

Ripoti nchini Uingereza zinasema kuwa Nadine, ambaye ni rais wa taasisi ya michezo ya Neymar nchini Brazil na anafuatwa na watu 1.6 milioni kwenye mtandao wake wa Instagram, alichukua hatua ya kutema mwanamitindo huyo kwa jina Tiago Ramos alipopata habari alikuwa shoga.

Kwa mujibu wa gazeti la O Dia nchini Brazil, Nadine, 52, alimfurusha Tiago kwenye kasri lake mnamo Jumatano iliyopita baada ya kugundua kwamba bingwa huyo wa masuala ya teknolojia ya kompyuta aliwahi kuwa katika mahusiano mengi ya kimapenzi na wanaume wengine kabla ya kukutana kwao.

Mbali na kuhusiana kimapenzi na Mauro ambaye ni mpishi mkuu wa Neymar, Tiago aliwahi pia kuwa shoga wa Carlinhos Maia, mwanamume ambaye ni mwigizaji maarufu jijini Rio, Brazil.

Awali, Neymar alikuwa ameunga mkono uhusiano mpya wa Nadine baada ya mamaye huyo kusisitiza kwamba hakuna yeyote ambaye angeelewa raha aliyokuwa akipata kutoka kwa Tiago ambaye ni gwiji wa miereka ya chumbani.

Japo Nadine amefichua kiini cha kumtema Tiago, gazeti la The Sun limesisitiza kwamba mama huyo alishinikizwa na familia yake kuchukua hatua hiyo baada ya kuwatia aibu kwa kuhusiana kimapenzi na kijana ambaye kiumri, anatosha kuwa mwanawe namba tatu. Neymar anamshinda Tiago kiumri kwa miaka sita zaidi.

Tiago kwa sasa anaandamwa na kahaba Dianne Buswell japo matamanio yake ni kuwatambalia makahaba Thomas Imogen, Kendra Lust au Pamela Anderson aliyewahi kumfungulia duka mwanasoka Adil Rami wa Ufaransa.

Wiki mbili zilizopita, Tiago alipasua mbarika kuhusu uhusiano wa siri ambao amekuwa nao na Nadine. Akitumia mtandao wake wa Instagram, alipakia picha walizowahi kupigwa pamoja katika sehemu mbalimbali za burudani wakishiriki vileo na kuonyeshana mahaba motomoto.

Katika mojawapo ya picha hizo, Nadine alikuwa amekishika kidevu cha Tiago aliyekuwa akipapasa maziwa ya mama huyo huku akimpiga mabusu shavuni.

Kwa mujibu wa gazeti la UEL Esporte nchini Brazil, Tiago ni mpenzi kindakindaki wa masuala ya kompyuta na yuko katika kikosi cha 4K Easy kinachojulikana kwa umaarufu wa kuunda michezo ya kompyuta.

Nadine alitengana na Wagner Ribeiro ambaye ni baba na wakala wa Neymar mnamo 2016 baada ya kuishi pamoja katika ndoa kwa kipindi cha miaka 25.

Hadi alipoanza kulitomasa tunda la Nadine,Tiago ambaye ni mzawa wa mji wa Pernambuco nchini Brazil, alikuwa shabiki sugu wa Neymar huku akihudhuria takriban michuano yote iliyomhusisha nyota huyo wa zamani wa Barcelona.