Shirika laonya mvua haitaleta afueni ya haraka dhidi ya njaa

Shirika laonya mvua haitaleta afueni ya haraka dhidi ya njaa

NA SIAGO CECE

SHIRIKA la kimataifa la kutabiri hali ya hewa lililo chini ya muungano wa serikali za Afrika (ICPAC), limeshauri mataifa kutolegeza kamba katika kusaidia waathiriwa wa ukame hata msimu wa mvua unapotarajiwa kuanza mwezi ujao.

“Msimu wa mvua nyingi haumaanishi kuwa eneo la ukame litapata nafuu mara moja hasa katika maeneo ya Afrika Mashariki,” akasema Mkurugenzi wa ICPAK, Bw Guleid Artan.

Kulingana na Shirika la Kenya Red Cross Society, hali ya ukame bado ni mbaya katika kaunti 13 nchini.

Meneja wa hatua za dharura katika shirika hilo, Bw Venant Ndighila alisema idadi ya kaunti zinazokumbwa na ukame inatarajiwa kuongezeka katika siku zijazo.

“Tulipokea mvua mwezi Oktoba hadi Desemba kwa msimu wa mwaka 2021 lakini haikuwa ya kutosha. Ilitupa matumaini makubwa kwa namna ambayo tuliona kana kwamba hali inaimarika,” Bw Ndighila alisema.

Alikuwa akizungumza katika wadi ya Kifyonzo kaunti ya Kwale wakati wa uzinduzi wa mpango wa kukabiliana na dharura wa kusaidia familia wiki iliyopita.

You can share this post!

Vinara wa Kenya Kwanza wadai Uhuru anapoteza muda kuzuru...

Korti yagawia mume mali iliyoshikiliwa na mkewe wa zamani

T L