Shujaa mawindoni kulipiza kisasi Dubai 7s msimu mpya ukianza leo

Shujaa mawindoni kulipiza kisasi Dubai 7s msimu mpya ukianza leo

Na GEOFFREY ANENE

Shujaa itaanza msimu wake wa 20 kwenye Raga za Dunia za wachezaji saba kila upande ikihitaji kufanya kazi ya ziada katika Kundi B kutinga robo-fainali mjini Dubai hii leo.

Vijana wa kocha Innocent “Namcos” Simiyu watamenyana na Amerika (9.16am), Argentina (1.30pm) na Uhispania (4.02pm) katika kundi hilo ambalo timu mbili za kwanza zitaingia mduara wa nane-bora. Shujaa,

ambayo baadhi ya wachezaji wake matata ni Alvin Otieno na Johnstone Olindi, itajibwaga uwanjani bila ushindi dhidi ya Amerika na Uhispania katika mechi mbili zilizopita mjini Dubai. Ilichabangwa 26-14 mwaka 2014 na 21-19 mwaka 26-17 dhidi ya Amerika inayojivunia wakali Carlin Isles na Perry Baker.

Pia, Shujaa ilipoteza 26-19 mwaka 2018 na 22-19 mwaka 2019 dhidi ya Uhispania mjini Dubai. Wakenya watakutana na Argentina, wanaopigiwa upatu kunyakua tiketi moja ya robo-fainali kutoka kundi hili, kwa mara ya kwanza mjini Dubai baada ya karibu muondo mmoja.

You can share this post!

Mwendwa aponea ila hatarejea afisini FKF

Onyo la Man City kwa wapinzani wao Uefa

T L