JAGINA WA SPOTI: Shujaa wa soka ajitolea kukuza chipukizi mitaani

JAGINA WA SPOTI: Shujaa wa soka ajitolea kukuza chipukizi mitaani

NA PATRICK KILAVUKA

KIGOGO wa soka Athanas Obala “Obango” licha ya kuzaliwa nchini miaka 57 Uganda iliyotupa kisogo wakati mzazi wake alikuwa anafanya kazi katika Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya Afrika, waligura Kenya mwaka 1975 baada ya kupata uhamisho na akawa na mshawasha wa kuendelea kukuza talanta ya Kabumbu.

Hata hivyo, alipata elimu yake ya Msingi Shule ya Nsyambia, Uganda kabla kujiunga na Shule ya Msingi ya North Highridge, Nairobi na hatimaye, kupata nafasi ya elimu ya sekondari Shule ya Upili ya Equator High.

Kwa vile kiu ya kusakata boli ilikuwa inamsakama sana akiwa anaishi eneo la Ngara, alisajiliwa na timu ya Nairobi Tigers ambayo ilikuwa inashiriki Ligi ya Divisheni ya Nne mwaka 1980-82 akicheza kama kiungo.

Nyota yake ya jaha iliendelea kung’ara pale ambapo aliguria timu ya Firestone 1983-1984 ambayo ilikuwa inapiga ngarambe ya Ligi ya Daraja ya Pili mkoa wa Nairobi.

Hatua kwa hatua soka yake ilikuwa inanawiri na 1984 -1986 alipata fursa ya kuchezea timu ya Kenya Re- Insurance Co-operation ambayo ilikuwa inashiriki Ligi ya Kitaifa ya Supa Daraja ya Pili.

Ni wakati uo huo, alikuwa ameajiriwa na Shirika la Posta kama karani alipojumuishwa pia katika timu na kuichezea 1985-1986 chini ya Kocha wa mwenye tajriba Marshall Mulwa aliyemgundua zaidi talanta yake na kunasihi kwamba, kutokana na kimo kirefu, atamnoa kama difenda na kumchochea zaidi kwa kumhusisha katika mazoezi ya timu ya Harambee Stars kwani alikuwa anaifunza pia.

Mwaka 1987-1989 alipigia soka MVOA ambayo ilipambana katika Ligi ya Mkoa wa Nairobi Daraja ya Pili kabla kusajili na Posta Rangers 1990 iliyokuwa inashiriki Ligi ya Divisheni ya kwanza mkoa wa Nairobi.

Hatimaye, alijiunga na Shabana ya Kisii ambayo ilikuwa inashiriki Ligi ya Kitaifa kwa miezi sita ambayo ilikuwa chini ya uenyekiti wa Bw Matundura, kocha Morris Ochieng ambaye aliiwezesha timu ya Gor Mahia pia kujishindia taji la Mandela Cup kabla kustaafu soka ya ushindani kutoka na jeraha la goti akisakatia timu hii.

Aliingilia ukocha 1995 ambapo alinoa timu kama Kangemi Youth, Leviticus na Coffee Board of Kenya kama naibu wa kocha chini ya Peter Basanga Otieno.

Mbali na ukufunzi wa Seychelles Marketing Board SMB (2003) – Ushelesheli, MVOA, Kangemi United ambayo ilicheza Ligi ya Kitaifa 2004-2005 kabla kupandishwa ngazi ya KPL 2006-’08 na kucheza kwa msimu mitatu.

Aliendela kujihusisha ya Kangemi United ilipoteremshwa Ligi ya Kitaifa chini ya Kocha Sammy Taabu kabla kuacha ukocha na kujiunga na usimamizi.

  • Tags

You can share this post!

Mimi niende Newcastle? Acheni hizo!

MATUKIO MUHIMU: Amefuzu ukocha viwango vya Fifa, KNVB na...

T L