Shujaa yanyoa Amerika ya kocha Mike Friday bila maji raga ya Dubai 7S II, Great Britain inasubiri katika fainali

Shujaa yanyoa Amerika ya kocha Mike Friday bila maji raga ya Dubai 7S II, Great Britain inasubiri katika fainali

Na GEOFFREY ANENE

KENYA Shujaa imetinga fainali ya nambari tano kwenye duru ya pili ya Raga za Dunia ya Dubai Sevens baada ya kuaibisha Amerika 29-0 katika nusu-fainali ugani Sevens nchini Milki za Kiarabu, Jumamosi.

Vijana wa kocha Innocent “Namcos” Simiyu walianza maangamizi hayo kupitia kwa Jeffrey Oluoch dakika ya pili, mguso ambao ulipatikana Kenya ikiwa chini wachezaji sita baada ya Johnstone Olindi kulishwa kadi ya njano ya kukalishwa nje dakika mbili.

Olindi alirejea kwa kishindo alipokamilisha adhabu yake alipopokonya mchezaji wa Amerika mpira na kutimka hadi katika kisanduku cha miguso dakika ya tano. Anthony Omondi aliongeza mkwaju wa mguso huo na kupatia Kenya uongozi wa alama 12-0 wakati wa mapumziko.

Skramu ya Kenya baada ya Amerika kuanzisha kipindi cha pili vibaya ilishuhudia Shujaa ikiimarisha uongozi wake hadi 17-0 kupitia kwa mguso wa Alvin “Buffa” Otieno dakika ya nane. Omondi aliongeza mkwaju wa mguso huo kabla ya kupachika miguso miwili katika dakika tatu za mwisho kutunuku Kenya ushindi huo wa kwanza dhidi ya vijana wa Mike Friday baada ya vichapo vitatu mfululizo na mkubwa dhidi ya wapinzani hao tangu 33-14 mnamo Aprili 2018.

Kenya sasa itamenyana na Great Britain katika mechi ya kuamua nambari tano na sita itakayosakatwa saa kumi na dakika tatu jioni leo. Great Britain ilibwaga Ireland 24-19 katika muda wa ziada.

You can share this post!

Jinsi wanawake warembo wanavyotumiwa kuwapora madereva wa...

DOUGLAS MUTUA: Bara Afrika linaonewa kwa kugundua kirusi...

T L