Shule kufunguliwa kulingana na kalenda ya wizara

Shule kufunguliwa kulingana na kalenda ya wizara

Na SAMMY WAWERU

SHULE na taasisi zote za elimu nchini zitafunguliwa kwa mujibu wa kalenda ya Wizara ya Elimu, amesema Rais Uhuru Kenyatta.

Rais Kenyatta alitoa tangazo hilo Jumamosi, wakati wa maadhimisho ya Leba Dei, yanayosherehekewa Mei 1 kila mwaka.

“Shule na taasisi zote za masomo zitafunguliwa kwa mujibu wa kalenda ya Wizara ya Elimu,” akasema.

Zilifungwa Machi 2021, baada ya kuhudumu muhula mmoja, uliorejelewa Januari 2021 ili kuendeleza shughuli za masomo kalenda ya 2020.

Aidha, zilikuwa zimesalia kufungwa kwa muda wa miezi minane mfululizo, kufuatia mkurupuko wa ugonjwa wa Covid-19 nchini Machi 2020.

Kulingana na maelezo ya Rais Kenyatta, huenda zikafunguliwa mwanzoni mwa Mei 2021.

  • Tags

You can share this post!

Mgonjwa hospitalini kutembelewa na mtu mmoja pekee kwa siku

Wafanyabiashara Muthurwa waitaka NMS iwape maji safi