Habari Mseto

Shule mbili zafungwa Mombasa baada ya corona kusambaa

October 24th, 2020 1 min read

NA MOHAMED AHMED

Shule mbili za upili zimefungwa Kaunti ya Mombasa baada ya walimu na wanafunzi kupatikana na virusi vya corona. Shule ya Upili ya Tononoka na Star of the Sea zilifungwa Jumatatu kwa muda wa wiki mbili.

Ripoti za kuaminika ziliambi Taifa Leo kwamba watu nane walipatikana na virusi vya corona Tononoka huku wengine wanne wakipatikana Star of the Sea.

Walimu kutoka shule hizo mbili ni kati ya walipatikana na vrusi vya corona.Mwalimu mkuu kutoka moja ya shule hizo ni kati ya wale walipatikana na virusi vya corona.

Ripoti zilisema kwamba walimu wenginee bado hawjapokea matokeo yao ya vipimo baada ya sampuli zao kuchukuliwa na maafisa wa afya.

“Waakati mwalimu mkuu alidhibitishiwa kuwa alikuwa na virusi vya corona hapo ndipo tuliombwa kupimwa zote.Matokeo ya vipimo yalikuja Jumatatu yakionyesha kwamba walimu na wanafunzi walikuwa wameambukizwa virusi vya corona,”zilisema duru za kuaminika.

Afisa mkuu kutoka serikalini alitembelea moja ya shule hiyo na kuagiza ifungwe hadi Novemba 2.

Brua iliyotumiwa wazazi na shule ya Star of the Sea ilisema kwamba masomo yamesitishwa kwa muda ili kuruhusu shule hiyo kunyunyuziwa dawa.