Habari Mseto

Shule mitaani sasa zakodishwa

August 13th, 2020 1 min read

SAMMY KIMATU na FAUSTINE NGILA

BAADHI ya shule kwenye mitaa ya mabanda Nairobi zimegeuza madarasa kuwa vyumba vya kukodisha kwa sababu ya janga la corona.

Kwenye shule ya Rock Academy kwenye mtaa wa mabanda wa Mukuru –Hazina eneo bunge ya Starehe tayari wakazi wamaishi kwenye madarasa hayo.

“Niliamua kukodisha vyumba hivyo ili tuweze kujimudu ,” alisema Bi Christine Kathukya, mkurugenzi.

Serikali iligangaza kufungwa kwa shule zote mwezi Machi baada ya kuzuka kwa janga la corona.Tangu huo wakati walimu wengi wamepoteza njia ya mapato. Wamiliki wa shule za kibinafsi wanapambana na kulipa deni za kodi.

Serikali ilitangaza kwamba shule zitarejea mwaka ujao.