Habari Mseto

Siagi zaidi ya Nuteez yapatikana na aflatoxin

February 7th, 2019 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Aina tatu zaidi za siagi ya njugu zimepatikana kutofaa kwa binadamu. Tangazo hilo lilitolewa siku kadhaa baada ya serikali kutangaza kuwa siagi ya Nuteez ilikuwa na kuvu sumu kiwango cha juu sana.

Aina za hivi sasa ni Mother Nature, Clover Nuts smooth na Clover Nuts chocolate ambazo zilipatikana kupitisha viwango vya kuvu sumu ambayo haiwezi kuathiri afya ya binadamu.

Viwango vya mwisho vya kuvu sumu vinafaa kuwa ni sehemu 10 kwa bilioni moja, lakini aina hizo zilipatikana kuwa na kuvu sumu kiwango cha 27.26 ppb, 36.44 ppb, na 44.25 ppb kwa mfuatano huo.

Afisi ya kutathmini ubora wa bidhaa (KEBS) katika taarifa ilisema imeondoa idhini ya kutengenezwa na kuuzwa kwa bidhaa hizo.

Watengenezaji wa bidhaa hizo pia walitakiwa na kuondoa bidhaa hizo sokoni. KEBS pia ilisema imetwaa siagi yote ya njugu katika kampuni ya Jetlak, ambayo hutengeneza Nuteez.