• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 8:50 AM
Atakayechukua nafasi ya Sabina Chege kutajwa katika PG ya Azimio

Atakayechukua nafasi ya Sabina Chege kutajwa katika PG ya Azimio

NA CHARLES WASONGA

KIONGOZI wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Opiyo Wandayi ametangaza kuwa ni kwenye mkutano wa kundi la Wabunge wa Azimio (PG) unaofanyika leo Jumanne, Mei 30, 2023 ambapo watataja atakayeteuliwa awe Naibu Kiranja wa Azimio katika Bunge la Kitaifa kuchukua mahala pa mbunge mbunge maalum Sabina Chege.

Kwenye kikao na wanahabari katika majengo ya bunge mnamo Jumatatu, Bw Wandayi ambaye ni Mbunge wa Ugunja alisema kuwa kikao hicho cha PG pia kitatoa maamuzi makali kuhusu adhabu kwa wabunge wa Azimio walioamua kushirikiana na mrengo wa Kenya Kwanza.

“Mkutano huo wa PG ambao tunahimiza wabunge wetu wauhudhurie bila kuchelewa pia utaafikiana kuhusu yule ambaye atachukua nafasi ya Sabina Chege ambaye ameasi muungano na sasa anaendesha mapinduzi ndani ya Jubilee,” akasema.

Mnamo Mei 4, wabunge wa Azimio waliondoka bungeni kwa hasira baada ya Spika Moses Wetang’ula kudinda kuidhinisha kuondolewa kwa Bi Chege.

Spika huyo alisema kuwa mrengo wa Azimio haukufuata sheria za bunge zinazosema kuwa chama cha kisiasa kinaweza kubadilisha uongozi wake bungeni. Kwa mujibu wa Bw Wetang’ula, Bw Wandayi aliyewasilisha ombi la kumtaka aidhinishe kutimuliwa kwa Bi Chege alipaswa kuwasilisha jina la mbunge atakayechukua nafasi hiyo.

Bw Wandayi alifeli hitaji hilo la sehemu ya 20 (5) ya sheria zinazoongoza shughuli za Bunge la Kitaifa.

Wakati wa mkutano wa wajumbe wa Jubilee iliamuliwa kuwa Mbunge wa Embakasi Magharibi Mark Mwenje ndiye anafaa kuteuliwa naibu kiranja wa wachache katika Bunge la Kitaifa.

  • Tags

You can share this post!

Mhubiri kutoka Nigeria ashtakiwa kwa kupora benki mamilioni...

Delmonte yawapiga jeki wasichana wa Mwana Wikio kwa kuwapa...

T L