• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 6:27 PM
Atwoli akashifu viongozi wachochezi

Atwoli akashifu viongozi wachochezi

Na STANLEY NGOTHO

KATIBU Mkuu wa Muungano wa Wafanyakazi Nchini (COTU) Francis Atwoli ametoa wito kwa Wakenya wakatae kuwachagua wagombeaji wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) akisema viongozi wake wanatoa matamshi ya uchochezi.

Akiongea na wanahabari Jumapili nyumbani kwake katika eneo la Ildamat, eneobunge la Kajiado ya Kati, Bw Atwoli alitaja Naibu Rais William Ruto kama kiongozi anayehusudu ukabila kwa lengo la kuwagawanya Wakenya.

Alimkashifu Dkt Ruto kwa kutumia wandani wake kuhubiri machafuko.

“Sharti Wakenya wamnyime Naibu Rais nafasi ya kutwaa urais. Amezingirwa na wahalifu ambao wajibu wao mkubwa ni kuchochea vita na uhasama,” akasema Bw Atwoli huku akibashiri kwamba Dkt Ruto atashindwa katika uchaguzi mkuu ujao.

Mfuasi huyo mkubwa wa kiongozi wa ODM Raila Odinga alisema matamshi ya uchochezi yaliyotolewa na Seneta wa Meru Mithika Linturi yanaakisi fikra za wabunge wanaoegemea chama cha UDA.

Bw Atwoli alisema matamshi hayo yanaweza kutumbukiza taifa hili katika machafuko, akisema kila Mkenya ana haki ya kuishi popote na kuunga mkono chama fulani cha kisiasa.

“Seneta Linturi anafaa kuadhibiwa kwa matamshi yake ambayo yanaweza kurejesha taifa hili katika machafuko ya kisiasa ya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007. Asasi za serikali zinafaa kuwadhibiti wanasiasa hawa wanaochochea ghasia,” akaongeza.

  • Tags

You can share this post!

Sabina Chege akana kuhamia Chama cha Kazi

TUSIJE TUKASAHAU: Walimu wakuu wapuuza mwongozo, waendelea...

T L