• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 1:05 PM
Kioni, Murathe warudishwa katika uongozi wa Jubilee

Kioni, Murathe warudishwa katika uongozi wa Jubilee

NA RICHARD MUNGUTI

KATIBU Mkuu wa chama cha Jubilee Jeremiah Kioni aliyefurushwa na kundi la mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Kanini Kega, amepata afueni baada ya kurudishwa katika uongozi wa chama cha Jubilee.

Jopo la kuamua mizozo ya vyama vya kisiasa limemwamuru msajili wa vyama vya kisiasa Ann Nderitu asitambue uongozi wa Bw Kega ambaye majuma kadhaa yaliyopita alitangaza kumvua uongozi Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta na kusema mbunge maalum Sabina Chege ndiye angekuwa kiongozi wa chama.

Jopo hilo pia limeagiza David Murathe arudishwe kwa wadhifa wa Naibu Mwenyekiti wa chama hicho huku naye Kagwe Gichohi akirudishwa awe mwekahazina wa kitaifa.

Jana Jumatatu Bw Kenyatta aliongoza viongozi wengine wa Jubilee kuandaa Kongamano la Kitaifa la Wajumbe (NDC) katika ukumbi wa Ngong Racecourse ambapo alisema kunyamaza kwake hakumaanishi yeye ni mwoga.

“Sisi ni watu wanaopenda amani. Kukumbatia amani hakumaanishi sisi ni waoga. Hutatusikia tukitusi mtu,” akasema Rais huyo mstaafu ambaye alimkabidhi Dkt William Ruto madaraka mnamo Septemba 13, 2022.

  • Tags

You can share this post!

PATA USHAURI WA DKT FLO: Nahisi maumivu kila ninapoenda...

Mahakama Kuu yaonya jopo la uchunguzi Shakahola

T L