• Nairobi
  • Last Updated December 8th, 2023 10:25 PM
Mchakato wa kumtimua Nyaribo waanza mzozo ukichacha

Mchakato wa kumtimua Nyaribo waanza mzozo ukichacha

NA WYCLIFFE NYABERI

MCHAKATO wa kumuondoa afisini Gavana wa Nyamira Amos Nyaribo umeanza kushika kasi.

Hii ni baada ya madiwani kuarifiwa kuwa mswada wa kumtimua utawasilishwa wiki ijayo.

Spika wa Bunge la Kaunti ya Nyamira Enock Okero, amewaeleza madiwani wa Nyamira kuwa Ijumaa ijayo, watakuwa na kikao maalum kitakachojadili jinsi ya kumng’atua mamlakani gavana Nyaribo.

“Kutakuwa na kikao maalum Ijumaa, Septemba 22, 2023 kuanzia saa tatu na nusu asubuhi katika Bunge la Kaunti. Shughuli ya siku hiyo itakuwa ni kutoa notisi ya mswada wa kumuondoa afisini gavana Nyaribo,” ilisema sehemu ya taarifa ya Spika huyo kwa madiwani wake.

Mzozo kati ya gavana Nyaribo na madiwani hao unatokana na hatua ya Nyaribo kumwachisha kazi aliyekuwa Waziri wake wa Afya Timothy Ombati kwa kudai kuwa waziri huyo alihusika kwenye ufujaji wa pesa zilizohitajika kununua dawa katika hospitali za Nyamira.

Waziri huyo alifutwa kazi baada ya kutumikia likizo ya lazima ya siku 30.

Hatua hiyo iliwakera mno baadhi ya madiwani waliodai kuwa Bw Ombati alitolewa kafara katika sakata kubwa ya ufisadi katika serikali ya Nyaribo.

Wakiongozwa na mwenzao wa Ekerenyo Thaddeus Nyabaro, madiwani hao pia walidai Nyaribo alimfuta Ombati kwa kuwa hatoki katika ukoo wake.

Madiwani hao walipotisha kuwa watamng’atua Nyaribo afisini mara ya kwanza, gavana huyo alishikilia kuwa “siwezi kuogopa vitisho vyao”.

  • Tags

You can share this post!

Shujaa yajikatia tiketi ya robo-fainali Kombe la Afrika

Wanahabari wafukuzwa wakifuatilia stori ya moto shuleni...

T L