• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 6:55 AM
Ni rasmi Sabina Chege amevuliwa wadhifa wa Naibu Kiranja wa Wachache

Ni rasmi Sabina Chege amevuliwa wadhifa wa Naibu Kiranja wa Wachache

NA CHARLES WASONGA

HATIMAYE Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula ameidhinisha uamuzi wa muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya wa kumpokonya Mbunge Maalum Sabina Chege wadhifa wa Naibu Kiranja wa Wachache.

Nafasi yake sasa imechukuliwa na Mbunge wa Embakasi Magharibi Mark Mwenje aliyeteuliwa na chama cha Jubilee na kuidhinishwa katika mkutano wa kundi la wabunge wa muungano huo Mei 28, 2023.

Kwenye uamuzi alioutoa Jumatano alasiri, Bw Wetang’ula alisema kuwa hatua hiyo ni halali kwa sababu ilifikiwa kwa mujibu wa sheria za bunge hilo.

“Kwa msingi huu, Mark Mwenje anachukua nafasi ya mbunge maalum Sabina Chege kama Naibu Kiranja wa Wachache,” akasema kwenye taarifa aliyoitoa kwa kamati ya bunge lote mwendo wa saa tisa alasiri.

  • Tags

You can share this post!

Mwanamume ashtakiwa kujifanya wakili na kumwakilisha Sheng...

Jenerali wa Mawaziri? Moses Kuria ataka aletewe malalamishi...

T L