• Nairobi
  • Last Updated June 12th, 2024 4:24 PM
Obure naye atangaza kugombea ugavana Kisii

Obure naye atangaza kugombea ugavana Kisii

Na RUTH MBULA

KINYANG’ANYIRO cha ugavana kaunti ya Kisii kinaendelea kuvutia wagombeaji zaidi baada ya waziri msaidizi wa wizara ya uchukuzi Chris Obure kutangaza azma ya kumrithi Gavana James Ongwae.

Obure, 76, alikuwa wa pili katika uchaguzi wa 2017 nyuma ya Bw Ongwae aliyeshinda kuhudumu kwa muhula wa pili.

Kiti hicho kimevutia wagombeaji 10 wakiwemo mibabe wa siasa katika kaunti hiyo.

Baadhi ya wanaomezea mate kiti hicho ni mbunge wa Dagoreti Kaskazini Simba Arati, Seneta Sam Ongeri, naibu gavana Joash Maangi na mwakilishi wa wanawake katika kaunti hiyo Janet Ong’era watakaomenyania tiketi ya chama cha ODM.

Wengine ni wabunge Manson Nyamweya (Mugirago Kusini) na Ezekiel Machogu (Nyaribari Masaba), Bw Omingo Magara na Bw Charles Matoke.

You can share this post!

Mihadarati: Magoha aunga wanafunzi wapimwe

Man-United wapepeta Burnley na kurukia nafasi ya sita...

T L