• Nairobi
  • Last Updated May 24th, 2024 2:08 PM
Raila kukaribishwa kwa heshima na taadhima atakaporejea kutoka Dubai

Raila kukaribishwa kwa heshima na taadhima atakaporejea kutoka Dubai

NA CHARLES WASONGA

KIONGOZI wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga anatarajiwa kupewa makaribisho ya heshima na taadhima Ijumaa atakaporejea kutoka ziara ya Dubai.

Mara tu atakapotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), msafara wake utafululiza hadi katika uwanja wa Kamkunji, Kibra ambapo atahutubia mkutano wa Azimio almaarufu People’s Baraza.

“Kwa hivyo tunahimiza wafuasi wetu wanaounga mkono azma yetu ya kupigania taifa letu kuwa lenye misingi ya uwazi na demokrasia na linalojali raia, wajitokeze kwa wingi mkaribisha Bw Odinga na wahudhurie mkutano wa hadhara Kibra. Vile vile kila mmoja atakayehudhuria, tunahimiza kwamba afanye hivyo kwa amani bila vurugu,” amsesema Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Opiyo Wandayi.

Mrengo wa Azimio umepanga kurejelea maandamano mnamo Mei 02, 2023.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Nguzo kuu ya dini ni utu bali si maisha ya baada...

Mhuburi alilenga hasa wanafamilia

T L