• Nairobi
  • Last Updated May 28th, 2023 7:20 PM
Sabina Chege akana kuhamia Chama cha Kazi

Sabina Chege akana kuhamia Chama cha Kazi

Na KENYA NEWS AGENCY

MWAKILISHI wa Kike katika Kaunti ya Murang’a, Bi Sabina Chege, amekanusha madai ya kuhama kutoka Chama cha Jubilee (JP) na kujiunga na Chama Cha Kazi (CCK), kinachohusishwa na mbunge Moses Kuria (Gatundu Kusini).

Akizungumza katika Taasisi ya Mafunzo ya Kiufundi ya Michuki, Murang’a, Jumamosi, Bi Chege alitaja madai hayo kuwa uwongo unaoenezwa na watu wenye nia mbaya dhidi yake.

Alisema atatangaza mwelekeo wake wa kisiasa kuhusu chama na nafasi ambayo atawania kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti.

Hata hivyo, alikubali kwamba kumekuwa na wito kwa viongozi wakuu wa Jubilee kuboresha upya chama hicho.

  • Tags

You can share this post!

KCSE: Magoha aahidi ‘huruma’ kwa watahiniwa

Atwoli akashifu viongozi wachochezi

T L