• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 6:55 AM
Sakaja akodolea macho mikosi iliyomwandama Sonko

Sakaja akodolea macho mikosi iliyomwandama Sonko

NA WINNIE ONYANDO

LICHA ya wandani wa Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja kupata afueni, nyufa ndani ya United Democratic Alliance (UDA) na vuta nikuvute baina ya pande mbili hasimu za madiwani wa chama hicho ni tishio kwa utawala wake katika jiji kuu.

Mnamo Jumanne, washirika wa Sakaja walipata afueni baada ya Jopokazi la kutatua mizozo ya vyama vya kisiasa kusimamisha utekelezaji wa mabadiliko ya uongozi yaliyofanywa na UDA.

Hii ni baada ya washiriki hao wa Sakaja ambao ni Antony Kiragu-kiongozi wa wachache katika bunge la kaunti na kiranja wa wachache katika bunge hilo, Bw Mark Mugambi kuwasilisha ombi la kulitaka jopokazi hilo kuzuia utekelezaji wa mabadiliko hayo.

Mwenyekiti wa jopokazi hilo, Desma Nungo alitoa agizo la muda la kuzuia UDA na Bunge la Kaunti ya Nairobi kutekeleza uamuzi huo, ikisubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa ombi hilo.

Kesi hiyo itatajwa Novemba 7, 2023, saa nane unusu kwa maelekezo zaidi.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya Katibu Mkuu wa chama cha UDA Cleophas Malala kupitia taarifa kwa vyombo vya habari kumteua diwani wa Nairobi Kusini Waithera Chege kuchukua nafasi ya Bw Kiragu huku nafasi ya diwani wa Umoja One Mark Mugambi ikichukuliwa na diwani Joyce Muthoni.

Wawili hao walitolewa kwa tuhuma za kushindwa kuwaunganisha madiwani wa mrengo wa UDA.

Bi Waithera ndiye aliyewaongoza madiwani hao katika mchakato wa ukusanyaji wa sahihi ya kuwaondoa uongozini madiwani hao.

Kadhalika, madiwani hao pia walisema kuwa viongozi hao wameshindwa kuwawakilisha vyema bungeni na kwamba wawili hao ni wabadhirifu.

Kando na hayo, Bw Kiragu na mwenzake ni wandani wa Sakaja na wamekuwa wakishirikiana naye kikazi.

  • Tags

You can share this post!

Kaeni chonjo watoto wasizame kwa filamu chafu za ngono,...

Chimbuko la desturi ya wanawake wa Kiislamu kutenganishwa...

T L