• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 11:55 AM
UCHAMBUZI: Miaka 10 baadaye Ruto azuru The Hague akiwa Rais wala sio mshukiwa wa uhalifu wa kibinadamu

UCHAMBUZI: Miaka 10 baadaye Ruto azuru The Hague akiwa Rais wala sio mshukiwa wa uhalifu wa kibinadamu

NA CHARLES WASONGA

RAIS William Ruto mnamo Jumatatu, Mei 8, 2023, alirejea jijini The Hague, nchini Uholanzi akiwa Kiongozi wa Nchi, miaka 10 baada ya kufika huko akiwa mshukiwa wa uhalifu dhidi ya binadamu kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007.

Dkt Ruto alifika katika jijini The Hague ambako ndiko kuna Mahakama ya Kimataifa kuhusu Uhalifu (ICC), mwaka wa 2013, akiwa Naibu Rais.

Rais Ruto alishtakiwa pamoja na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, aliyekuwa Mkuu wa Utumishi wa Umma Francis Muthaura, aliyekuwa Mbunge wa Tinderet Henry Kosgei, aliyekuwa Kamishna wa Polisi Hussein Ali na aliyekuwa mtangazaji wa Kass FM Joshua arap Sang.

Rais Ruto yuko nchini Uholanzi kwa ziara rasmi ya siku mbili.

Jumatatu Rais Ruto alikutana na Mfalme wa Uholanzi Willem-Alexander na Malkia Maxima katika kasri la Noordeinde.

Wakati wa mkutano huo, kiongozi wa taifa alisema Kenya inathamini uhusiano mzuri kati yake na Uholanzi.

Rais Ruto na Mfalme Willem-Alexander walielezea kujitolea kwa kuimarisha uhusiana huo haswa katika nyanja ya kibiashara na kidiplomasia kwa manufaa ya raia wa nchi hizi mbili.

Kenya huuza mazao kama vile mboga na matunda, bidhaa za mifugo, chai, kahawa, maua, samaki miongoni mwa bidhaa nyinginezo.

Rais Ruto na Mfalme huyo wa Uholanzi pia walijadili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na juhudi ambazo Kenya inaweza katika uhalifu wa wanyamapori.

Mfalme Willem alisema Uholanzi itaendelea kuisaidia Kenya kustawisha maeneo kame, kufadhili miradi ya maji na usafi wa mazingira, afya, miundomsingi na utafiti wa kilimo.

  • Tags

You can share this post!

Viongozi sasa waomba Gavana Natembeya ‘atembee...

Msichange pesa kwa kila ‘tatizo’ mnalosikia...

T L