• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
Wana walioadhibiwa ODM warudi Ikulu kupata mawaidha ya Rais Ruto

Wana walioadhibiwa ODM warudi Ikulu kupata mawaidha ya Rais Ruto

NA MWANDISHI WETU

SENETA wa Kisumu Profesa Tom Ojienda na wabunge waliochukuliwa hatua za kinidhamu na chama cha Orange Democratic Movement (ODM) wamehudhuria kikao kilichoongozwa na Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi mnamo Jumatano.

Prof Ojienda na wabunge Gideon Ochanda (Bondo), Elisha Odhiambo (Gem), Phelix Odiwuor (Lang’ata), Mark Nyamita (Uriri), Caroli Omondi (Suba Kusini) na Paul Abuor (Rongo) ambao wanachukuliwa kuwa waasi, wamechukua hatua hiyo wiki moja baada ya ODM inayoongozwa na Raila Odinga kuwaadhibu.

Seneta wa Kisumu pamoja na wabunge wanne isipokuwa Bw Nyamita na Bw Abuor, walitimuliwa chamani ODM. Hata hivyo, mnamo Jumanne Jopo la Kutatua Mizozo ya Vyama vya Kisiasa (PPDT) ilipiga ODM breki kali.

Taarifa kutoka kwa kikao hicho cha Ikulu imesema wameangazia masuala manne makuu.

“Kwanza kwa niaba ya wakazi wa Nyanza tunaishukuru serikali kwa kuchukua hatua madhubuti kufufua sekta ya sukari. Tutaunga mkono mswada wa sukari utakaowasilishwa bungeni kesho Alhamisi,” ikasema sehemu ya taarifa hiyo.

Pia wamejadili suala la kuanza kwa safari za ndege hadi Migori na wakamualika Rais kutembelea eneo la Luo Nyanza kwa ziara ya kikazi.

Mwisho wamesisitiza wataendelea kuiunga mkono serikali kwa ajili ya ufanikishaji wa maendeleo katika maeneo yao ya uwakilishi na kote nchini.

  • Tags

You can share this post!

Wakulima Homa Bay wasusia mbolea ya bei nafuu

Mcharaza gita Lokassa ya Mbongo akosa kuzikwa miezi sita...

T L