Makala

SIHA NA LISHE: Pilipili zina faida lakini pia madhara yapo

June 1st, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

PILIPILI inasaidia sana kusawazisha kiwango cha sukari kwenye damu. Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene au wanaougua ugonjwa wa kisukari.

Pilipili husaidia kupunguza uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata nafuu.

Vilevile kiungo hiki husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja ya mwili.

Pilipili husaidia kufungua kwa haraka mianzi ya pua zilizoziba kwa mafua na kumfanya mtu kupumua kwa urahisi zaidi.

Kula pilipili kunasaidia kupunguza lehemu mwilini.

Madhara ya pilipili

Usitumie pilipili kutibu kifua. Kiungo hiki kinapoliwa na mgonjwa mwenye matatizo ya kifua humsababishia kukohoa mara mbili zaidi ya hapo awali.

Kutokana na mwasho, kiungo hiki huingia moja kwa moja kwenye mapafu na kusababisha kukohoa zaidi ambako kunaweza kuleta madhara ya mgonjwa kukohoa damu.

Pia kiungo cha pilipili husababisha ugonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa ambao hupenda pilipili kwa wingi. Elewa kuwa utumbo ni laini sana hivyo ni vizuri kuutunza hasa katika matumizi ya vyakula vyenye pilipili kiwango kidogo.