SIHA NA LISHE: Ukitaka protini kula vyakula hivi

SIHA NA LISHE: Ukitaka protini kula vyakula hivi

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

Kazi za protini mwilini

• protini ni muhimu katika kujenga mwili

• ni muhimu kwa sababu hufanya vidonda na majeraha kupona

• kutengeneza kinga za mwili au kingamwili

• kutengeneza chembechembe za seli nyekundu za damu

• kutengeneza enzymes zinazotumika katika kumeng’enya chakula

• kutengeneza homoni muhimu mwilini

• huhusika katika kutengeneza tishu – nyama na misuli – ndani ya mwili

Samaki

Samaki ni chanzo kizuri cha protini. Samaki wenye mafuta kama salmon ni vyanzo vyema zaidi vya protini.Pia ulaji wa samaki ni muhimu kwa afya ya ubongo, kukinga mwili dhidi ya maradhi mbalimbali, chanzo cha madini ya chumvi na mafuta.

Samaki. Picha/ Margaret Maina

Mayai

Mayai yanayotagwa na kuku yamesheheni protini. Watu wengi hupata protini kwa kula mayai. Unaweza kula yai likiwa ama limekaangwa au kuchemshwa.

Maziwa

Maziwa ni chanzo muhimu cha protini kwa binadamu na wanyama. Maziwa ya mama ni chanzo ambacho ni cha kipekee kilicho salama zaidi kwa mtoto mchanga kuliko hata yale ya ng’ombe. Mbali na kutupatia protini, maziwa pia ni chanzo cha vitamini. Maziwa ni bidhaa iliyo katika kategoria ya vyakula vilivyokusanya viinilishe vyote muhimu. Ni vyema kuyachemsha maziwa kabla ya kuyanywa ili kuepuka baaadhi ya matatizo ya kiafya.

Maziwa yakiwa katika kibuyu. Picha/ Margaret Maina

Nyama

Tunaweza kupata protini kwa kiasi kikubwa kwa kula nyama. Inaweza kuwa nyama nyekundu ama nyama nyeupe. Nyama nyeupe ni kama kuku na samaki. Nyama nyekundu ni ile inayotokana na mbuzi, kondoo na wanyama wengi wengineo.

Mimea jamii ya kunde na nafaka

Hii ni mimea ambayo inatambaa kama kunde na maharagwe na mimea ya jamii hii. Mimea hii inatambulika kuwa na kiasi kikubwa cha protini. Kwa watu wenye kipato cha chini, mimea hii ni chanzo cha msingi cha kupata protini. Maharagwe yapo ya aina nyingi. Ulaji wa aina zote hizi unaweza kutupatia protini.

You can share this post!

Afisa wa ODM apatikana na Covid-19

Walimu mjini Mombasa washtaki shule kwa kuwakata asilimia...

adminleo