Kimataifa

Sijaosha uume wangu kwa miaka 24, dume lafunguka

February 11th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MWANAMUME mchafu kupindukia kimwili na kitabia kutoka Uingereza alieleza daktari katika kipindi cha matibabu kuwa hajaosha uume wake kwa miaka 24, huku akiugua magonjwa ya zinaa kila mara.

Akizungumza katika kipindi kiitwacho E4 The Sex Clinic, mwanamume huyo alieleza mtangazaji kuwa hajaosha uume wake kwa muda huo, alipokuwa akieleza namna amekuwa na matatizo katika sehemu hiyo kama kuumwa nakatika njia ya mkojo na kupata magonjwa.

Maneno yake yaliwakasirisha watu wengi ambao waliingia kwenye mitandao ya kijamii kumkashifu kwa kuwa mchafu ajabu.

Alikuwa akieleza Dkt Naomi, mtangazaji wa kipindi hicho, kuhusu matatizo katika nyeti zake na jinsi amekuwa na shida nyingi anapotaka kuutumia.

Alisema kuwa amekuwa akihisi uchungu na mwasho kichwani mwa uume wake, na kuongeza kuwa kwa miezi tisa amekuwa akiugua magonjwa ya zinaa kama kaswende.

Mwanamume huyo ana umri wa miaka 24 na alisema kuwa hajawahi kuosha sehemu hiyo tangu azaliwe, na hivyo alishindwa angeaza kufanya hivyo namna gani.

Watazamaji wa kipindi hicho walishangaa na kuanza kufunguka mitandaoni.

“Ni wapi kweli hawa watu wa Sex Clinic huwapata watu hawa?” mmoja akauliza.

Kipindi hicho kimekuwa kikiangazia masuala ya kisiri kuhusu ngono Uingereza na kinalenga kuweka wazi mambo ambayo mbeleni yalichukuliwa kuwa mwiko.