Dondoo

Siku ya arobaini ya jamaa mhanyaji yatimia baada mke kupata kondomu kwa begi

June 1st, 2024 1 min read

NA JANET KAVUNGA

MWATATE, TAITA TAVETA

MWANADADA anayefunza katika shule moja eneo hili amekosa imani na mumewe baada ya kupata pakiti ya kondomu iliyofunguliwa kwenye begi alilotumia akiwa safarini.

Jamaa alirejea kutoka ziara ya kikazi na mkewe akaamua kutoa nguo begini ampe yaya afue alipopata pakiti hiyo ikiwa na kondomu moja, ishara kwamba mbili zilikuwa zimetumiwa.

Alipomuuliza mumewe ilikotoka pakiti hiyo, alimwambia aliiokota katika chumba cha hoteli aliyokuwa akiishi na kukanusha kabisa kuwa aliinunua na kutumia kondomu mbili kwa shughuli za michepuko.

“Sikumwamini kamwe japo nilifurahia aliweza kutumia kinga katika michepuko yake,” demu aliambia wenzake wakibadilishana maoni katika ukurasa mmoja wa mtandao wa kijamii wa akina dada.