Siku ya sarakasi kwa Wanjigi, alala ndani licha ya kujifungia kwa nyumba

Siku ya sarakasi kwa Wanjigi, alala ndani licha ya kujifungia kwa nyumba

Na RICHARD MUNGUTI

POLISI Jumanne walimkamata mfanyabiashara Jimmy Wanjigi na mkewe Irene Nzisa licha ya agizo la mahakama kuu wasiwatie nguvuni na kuwafungulia mashtaka.

Bw Wanjigi alikamatwa na kufululizwa moja kwa moja hadi kituo cha polisi cha Kamukunji atakapokesha kabla ya kupelekwa kortini.

Mfanyabiashara huyo alishikwa ilhali Jaji Antonty Mrima alikuwa ametoa agizo ikipinga kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Jaji Mrima aliamuru Inspekta Jenerali wa Polisi Hilary Mutyambi na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) wasimfungulie mashtaka Bw Wanjigi na mkewe Irene Nzisa.

Polisi waliwafurusha kutoka afisi za kampuni yao Kwacha Limited iliyoko Westlands Nairobi.

Jaji Mrima aliratibishwa kesi iliyowasilishwa na wakili Willis Otieno kuwa ya dharura kisha akaagizwa isikizwe Feburuari 9,2022.

Jaji Mrima pia alimwamuru Bw Otieno awakabidhi washtakiwa DPP, IG na Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai (DCI) nakala za kesi hiyo katikamuda wa siku tatu.

Jaji Mrima pia alimwamuru DPP asimshtaki Bw Wanjigi na Irene kuhusu umiliki wa shamba ambapo afisi za kampuni yao ya Kwacha Limited zimejengwa.

Ijapokuwa Mahakama kuu imewazima polisi kumfungulia mashtaka Bw Wanjigi, afisa mkuu kituo cha polisi cha Muthaiga alimshtaki Bw Wanjigi na mkewe Irene Nzisa kwa kula njama za ulaghai wa ardhi.

Cheti hicho cha mashtaka pia kimepigwa mihuri na afisi ya DPP na ile ya IG.

Mbali na Bw Wanjigi na mkewe Irene washukiwa wengine waliotajwa katika cheti hicho cha mashtaka ni Himanshu Velji Dodhia almaarufu kwa jina Himanshu Velji Premchard Dodhia, Kaneez Noorani ,Mohamed Hussein Noorani, Mohamed Hussanali, Kairu Augustine Thuo na John Nyanjua Njenga.

Shtaka dhidi yao lasema kati ya  Aprili 9,2010 na Juni 5,2018 wakishirikiana wote wanane walijitengenezea cheti feki cha umiliki wa shamba nambari IR65800 LR No1870/11/200.

Cheti cha usorovea wa shamba hilo ni Nambari 175145 kilichoandikishwa mnamo Julai 20 1993 kwa jina la kampuni ijuliknayo Horizon Hills Limited.

Shtaka la pili dhidi ya wanane hao lasema walijitengenezea cheti feki cha umiliki wa shamba la ukubwa wa 0.3314 hekitea kwa jina la  Dodhia Foam Limited, kampuni inayotengeneza godoro.

Wanadaiwa cheti hicho kilikuwa kimeidhinishwa na  Mwanasorevea G S Gitau.

Shtaka la tatu dhidi ya wanane hao lasema walighushi cheti cha umiliki wa shamba hilo wakidai ni halali kilichotiwa sahihi na aliyekuwa Kamishna wa Ardhi Wilson Gachanja.

Shtaka la nne ni dhidi ya  Wanjigi, mkewe Nzisa na Njenga wameshtakiwa kusababisha wakili wa Serikali katika afisi ya msajili wa kampuni kubadilisha katika cheti  cha usajili jina la Horizon Hills Limited kuwa Aureen Limited mnamo Mei 31 2018.

Mnamo Juni 2018 katika afisi za Wizara ya Ardhi Irene Nzisa mumewe Wanjigi na Njenga walimkabidi Bw Gachanja cheti cha umiliki wa shamba kwa jina  Dodhia Foam Limited wakidai kilikuwa halali.

Shtaka la sita dhidi ya Wanjigi , mkewe Irene Nzisa na Njenga ni la kupokea pesa kwa njia ya undanganyifu.

Wanashtakiwa kupokea Sh56milioni kutoka kwa kampuni ya Kenroid Limited wakidai walikuwa na uwezo wa kuiuzia shamba la hektari 0.3314 lililoandikishwa kwa jina la Aureem Limited. Hayo ndiyo mashtaka yanayomkabili Bw Wanjigi.

  • Tags

You can share this post!

Magavana waweka ‘bet’ yao kwa Raila

Mdalasini na faida zake mwilini

T L