Habari Mseto

Sikuiba Sh12 milioni, mzee ajitetea kizimbani

June 13th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MZEE mwenye umri wa miaka 72 alishtakiwa Jumanne kwa ulaghai wa Sh12 milioni.

Bw Kuldip Singh Jandu alikanusha mashtaka mawili ya kumlaghai Mfanya biashara Shamir Dharamshi Radia.

Shtaka lilisema Bw Jandu alitumia barua aliyodai iliandikwa na kutiwa saini na mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya ardhi Dkr Muhammad Swazuri mnamo Novemba 8, 2013.

Bw Jandu alikana kuwa alitumia barua hiyo kupokea kwa njia ya undanganyifu Sh12 milioni kutoka kwa Bw Radia akidai shamba la Karen lilikuwa lake na angelimuuzia.

Hakimu mwandamizi Bw Kennedy Cheruiyot alimwachilia kwa dhamana ya Sh600,000 pesa tasilimu.

Kesi itasikizwa Julai 9.