Habari Mseto

Simba Coach taabani kwa kunaswa ikisafirisha mifuko 8.5 milioni ya plastiki

October 23rd, 2018 1 min read

Na WINNIE ATIENO

HALMASHAURI ya Mazingira (Nema), imemuagiza meneja wa kampuni ya mabasi ya Simba Coach kuhojiwa, baada ya basi lao kupatikana likisafirisha mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku.

Mifuko hiyo ipatao milioni 8.5 ni ya tani 1.7 ilikuwa imeagizwa kutoka nchi jirani ya Tanzania na kusafirishwa hadi Mombasa na mfanyibiashara mmoja kutoka Mombasa.

Mkurugenzi wa Nema katika kaunti ya Mombasa, Bw Stephen Wambua na mwenzake anayesimamia eneo la Pwani Titus Simiyu mwagizaji wa mifuko hiyo bado hajakamatwa na polisi.

“Bado anasakwa lakini tumemuita meneja wa kampuni hiyo aje kutuelezea.”

kmarufuku humu nchini. Mji wa Mombasa ulikuwa msafi lakini waagizaji wa mifuko iliyopigwa marufuku wameanza tena kuleta mifuko,” akasema Bw Wambua.

Alisema waagizaji huficha mifuko hiyo kwenye mifuko ambayo inaruhusiwa kutumika kuwa vigumu kugundua kama zimefichwa.

Akihutubia waandishi wa habari katika kituo cha polisi cha Central huko Mombasa, Bw Wambua alionya mabasi dhidi ya kutumika kusarifisha bidhaa ghushi na zile zilizopigwa marufuku humu nchini.